Loading...

Ame Ally 'Zungu' kutua Simba

SIMBA inaendelea kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu baada ya kuripotiwa kuwa katika hatua ya mwisho kukamilisha usajiri wa mshambuliaji wa Azam FC, Ame Ali 'Zungu'.

Taarifa ambazo zimepatikina Ame atatua kwenye kikosi hicho wakati wowote kuanzia leo endapo klabu hizo zitakubaliana katika mazungumzo yanayoendelea.

Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Iddi, aliliambia Nipashe mazungumzo ya pande hizo mbili yanaenda vizuri na uwenda mambo yakakamilika hivi karibuni.

"Ni kweli Azam tupo kwenye mazungumzo na wenzetu Simba, wameomba kumsajili Ame lakini bado viongozi wapo kwenye mazungumzo yakikamilika tutatoa taarifa rasmi," alisema Jaffar.
Ame alijiunga na Azam mwaka jana akitokea Mtibwa Sugar kwa mkataba wa miaka miwili na kwa sasa amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake.


ZeroDegree.
Ame Ally 'Zungu' kutua Simba Ame Ally 'Zungu' kutua Simba Reviewed by Zero Degree on 7/25/2016 10:18:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.