Loading...

Azam yanukia manoti, yasajili kiungo toka Medeama.


KLABU ya Azam FC iko mbioni kusaini mkataba mpya na benki ya NMB baada ya ule wa awali kufikia ukingoni ambapo utamalizika mwezi ujao.


Azam ilisaini mkataba wa miaka miwili na NMB mwaka 2014 ambao ulitajwa kuwa na thamani ya Sh 2 bilioni ambapo sasa iko mbioni kuongeza kandarasi hiyo ambayo utaifanya iendelee kusumbua nchini.

Makamu Mwenyekiti wa Azam, Nassoro Idrissa ‘Father’ alisema wamefikia katika hatua nzuri ya mazungumzo na NMB na pengine wanaweza kusaini mkataba huo katika siku za usoni.

“Ni mazungumzo ya pande mbili hivyo siwezi kusema kama tunasaini leo ama kesho lakini kikubwa ni kwamba tuko katika hatua nzuri za kuongeza mkataba huo”, alisema.


kiungo Enock Agyei.

Katika hatua nyingine Azam imekamilisha usajili wa kiungo Enock Agyei kutoka Medeama ya Ghana usajili ambao Father ameutaja kuwa ni mwanzo wa kupata Azam bora.

Source: Mwanaspoti
ZeroDegree.
Azam yanukia manoti, yasajili kiungo toka Medeama. Azam yanukia manoti, yasajili kiungo toka Medeama. Reviewed by Zero Degree on 7/29/2016 11:22:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.