Loading...

Klabu ya Simba kuwa kampuni.

WAKATI wanachama wa Simba wakijiandaa kuingia kwenye utaratibu wa klabu kuendeshwa kwa mfumo wa kampuni, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema klabu hiyo itapata maendeleo iwapo itangia kwenye mfumo huo.

Akizungumza kwenye mahojiano na kituo kimoja cha radio Dar es Salaam, Nape alisema kuwa hatua ya kubadili mfumo utaifanya Simba ijiendeshe kisasa na kuharakisha mafanikio ambayo ndiyo kiu ya mashabiki na wanachama wa klabu hiyo.

"Mnaweza mkaiondoa klabu na kuipeleka kwenye kampuni, lakini ubabaishaji ukashindwa kuleta maendeleo, ni vizuri hata hao wanaotaka kuwekeza katika mfumo wa kisasa wasiwe wababaishaji, wanatakiwa wawe watu makini," alisema Nape.

Waziri huyo alisema ni vizuri kanuni na taratibu za mfumo huo mpya zikafuatwa ili kuepuka mambo yasiyoitajika ambayo huenda yakavuruga nia njema hiyo.
Wanachama wa Simba wanatarajiwa kufanya uamuzi wa kukubali au kukataa mabadiliko hayo katika mkutano mkuu utakaofanyika Jumapili kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay jijini.

ZeroDegree.
Klabu ya Simba kuwa kampuni. Klabu ya Simba kuwa kampuni. Reviewed by Zero Degree on 7/29/2016 10:44:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.