Loading...

Dk Mwaka afutiwa kibali cha utoaji tiba asili na tiba mbadala

Mmiliki wa Foreplan, Juma Mwaka.

Dar es Salaam. Serikali imekifungia kituo cha tiba asilia cha Foreplan kinachomilikiwa na Juma Mwaka kwa kukiuka masharti ya
kibali alichopewa kujitangaza kuwa anatoa tiba za kisasa badala ya matibabu ya asilia.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti Wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dk Edmund Kayombo amesema kuwa kituo hiko kimefutiwa usajili na hakiruhusu kutoa huduma za tiba asilia na tiba mbadala kwa jamii kwa kutokidhi masharti ya usajili na kufanya kazi kinyume cha usajili wake. 


Mwenyekiti Wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dk Edmund Kayombo.


“Kuanzia hivi sasa tumekifutia usajili kituo cha tiba asili na tiba mbadala cha Foreplan kwa kukiuka masharti ya usajili na hivyo hakiruhusiwi kutoa huduma kwa jamii na watanzania kwa ujumla,”amesisitiza Dk Kayombo.

Ameongeza kuwa vituo vingine vilivyofungiwa kutoa huduma ni pamoja na Tabibu Abdallah Mandai wa Mandai Herval Clinic na Kituo cha Fadhaget Sanitarium Clinic kinachomilikiwa na Tabibu Fadhil Kabujanja.

Habari zilizotangulia kuhusu Dk Mwaka na Foreplan Herbal:



ZeroDegree.
Dk Mwaka afutiwa kibali cha utoaji tiba asili na tiba mbadala Dk Mwaka afutiwa kibali cha utoaji tiba asili na tiba mbadala Reviewed by Zero Degree on 7/12/2016 08:04:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.