Loading...

Mitandao ya kijamii YAFUNGWA nchini Ethiopia.

Mnamo mwezi Juni mwaka huu iliripotiwa kuwa nchini Algeria mitandao ya kijamii ililazimika kuzimwa kwa siku kadhaa hususani Facebook na
Instagram ili kuzuia udanganyifu katika mtihani wa kitaifa wa shule za upili jambo lililopolelekea wananchi wengi kufurika katika ofisi za mitandao hiyo.

Tukio hilo limeripotiwa tena nchini Ethiopia ambapo mitandao yote ya kijamii imefunga baada ya maswali ya mtihani wa mwisho wa mwaka kusambaa mitandaoni mwezi uliopita.

Jambo hilo lilipelekea kuwa na kashfa ya kitaifa na hata kufutwa kwa usajili wa baadhi ya wanafunzi.

Mitandao ya Facebook, Twitter na Viber imefungwa tangu Jumamosi asubuhi.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, mitandao ya kijamii imekuwa tatizo kwa maisha ya mwanafunzi na hivyo basi Ethiopia imeamua kuifunga kwa muda mfupi.

Mitandao hiyo itaendelea kufungwa hadi hapo kesho kwa mujibu wa msemaji huyo.

Credit: trtworld
ZeroDegree.
Mitandao ya kijamii YAFUNGWA nchini Ethiopia. Mitandao ya kijamii YAFUNGWA nchini Ethiopia. Reviewed by Zero Degree on 7/12/2016 07:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.