Loading...

Mwalimu acharangwa mapanga.

Serengeti. Mwalimu wa Shule ya Msingi Geitasamo, Kata ya Rung'abure wilayani Serengeti Mkoa wa Mara, Raphael Charles (22) amenusurika kifo kwa kucharangwa mapanga kwa tuhuma za kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Ikorongo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Geitasamo, Marwa Meng’anyi amesema alikatwa mapanga na kaka wa mwanafunzi waliochukizwa na kitendo cha dada yao (jina linahifadhiwa) kukatishwa masomo kwa kupewa ujauzito.

Mwalimu huyo aliyefungua mashtaka kuhusu shambulia hilo na kupewa na namba ya jalada Mug/RB/2886/2016 (kujeruhi), amesema kunusurika kwake kulipatikana baada ya mmoja wa mafundi pikipiki waliokuwa eneo jirani kujitokeza kumsaidia.

Tukio la kushambuliwa kwa mwalimu huyo limekuja huku tayari madai ya kudaiwa kumpachika mimba mwanafunzi huyo yakiwa yamefikishwa mahakamani kwa shauri namba 82/2016 tangu Mei 13 mwaka huu.


Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Mwalimu acharangwa mapanga. Mwalimu acharangwa mapanga. Reviewed by Zero Degree on 7/12/2016 07:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.