Shirika la ndege [ ATCL ], kupata ndege mpya Septemba.
Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali imelipa Sh36 bilioni, sawa na asilimia 40 kwa ajili ya kununua ndege mbili za shirika la ndege la ATCL.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.
"Kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano tutahakikisha hatua za ununuzi wa ndege mpya zinafanyika kwa haraka ili kuweza kulifufua shirika letu la ndege na kuweza kuanza kutoa huduma za usafiri wa anga ifikapo mwezi Septemba mwaka huu," amesema
Waziri huyo ametoa kauli hiyo alipokuwa akikagua ujenzi wa uwanja wa ndege wa Dodoma na kusema kuwa ameridhishwa na maendeleo ya upanuzi wake.
"Mradi huu umetupa mfano kama tukijipanga vizuri hata kwenye miradi mingine tunaweza kutekeleza kwa haraka na ubora unaotakiwa, kwa upande wetu kama Serikali tutahakikisha uwanja huu unakamilika haraka ili kuruhusu ndege kubwa kuanza kutua," amesema.

ZeroDegree.
Shirika la ndege [ ATCL ], kupata ndege mpya Septemba.
Reviewed by Zero Degree
on
7/12/2016 07:24:00 PM
Rating: