Loading...

DAKTARI FEKI AKAMATWA Akijiandaa Kuhudumia Wagonjwa Mkoani Morogoro.

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Zakaria Benjamini mkazi wa Tungi Manispaa ya Morogoro baada ya kuingia hospitali ya rufaa kwa nia ya kufanya utapeli na kutaka kutoa huduma kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi hilo Ulrich Matei amesema mtu huyo ameshikiliwa na jeshi hilo kufuatia tuhuma zinazo mkabili na mara baada ya kubaini ukweli wa jambo hilo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Wakizungumza baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni walinzi na wauguzi waliomkamata mtuhumiwa huyo wameeleza namna hali ilivyokuwa huku muuguzi wa zamu akieleza utaratibu unaotumika kuwabaini wafanyakazi halali.


Source: Mtembezi
ZeroDegree.
DAKTARI FEKI AKAMATWA Akijiandaa Kuhudumia Wagonjwa Mkoani Morogoro. DAKTARI FEKI AKAMATWA Akijiandaa Kuhudumia Wagonjwa Mkoani Morogoro. Reviewed by Zero Degree on 7/12/2016 10:25:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.