Donald Ngoma awatia hofu waghana.
Klabu ya Medeama ya Ghana imeeleza wazi kuwa kati ya safu ambayo wanahitaji kujipanga zaidi ni safu yao ya ulinzi kwa ajili ya kuwadhibiti mastraika wa Yanga Mzimbabwe, Donald Ngoma na Mzambia, Obrey Chirwa.
Waghana hao wamekiri kuwa Yanga ni timu nzuri lakini wamebaini kuwa wanabadilika zaidi pale mpira unapokuwa kwa mastraika wao hao, hivyo watajizatiti kuwazuia ili wasiwaletee shida wakiwa kwao.
Straika Donald Ngoma alifanikiwa kufunga bao la kuongoza katika dakika ya pili ya mchezo katika mechi iliyochezwa hivi karibuni Uwanja wa Taifa, Dar es Salam kabda ya Bernard Danso wa Medeama kurudisha bao hilo dakika ya 18.
“Ni kweli Yanga ni wazuri sehemu nyingi lakini mastraika wao wawili, yule Ngoma na aliyevaa namba 7 (Chirwa) ni wazuri sana. Hao ndiyo tunaotakiwa kucheza nao sana katika mechi yetu ya marudiano, hatutaki watusumbue, tukiwazuia hao, tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa,” alisema straika wa Medeama, Bismark Oppong.
Straika Donald Ngoma alifanikiwa kufunga bao la kuongoza katika dakika ya pili ya mchezo katika mechi iliyochezwa hivi karibuni Uwanja wa Taifa, Dar es Salam kabda ya Bernard Danso wa Medeama kurudisha bao hilo dakika ya 18.
ZeroDegree.
Donald Ngoma awatia hofu waghana.
Reviewed by Zero Degree
on
7/26/2016 11:20:00 AM
Rating: