Fainali ya kombe la EURO 2016 kuchezwa leo; Ufaransa wataka rekodi huku Ureno wakisaka heshima.
Paris, Ufaransa. Wenyeji wa michuano ya Euro 2016, Ufaransa watakwaana na Ureno katika mechi ya fainali itakayochezwa Stade de France huku kipa na nahodha wake, Hugo Lloris akisema fainali za mwaka huu zimewaweka salama na mashambulizi ya kigaidi.
Fainali hiyo itachezwa kwenye uwanja ambao waliwafunga Ujerumani katika mechi ya kirafiki miezi nane iliyopita baada ya kutokea milipuko ya kigaidi iliyoua watu 130 huku mamia wakijeruhiwa.
Ufaransa iliingia fainali baada ya kuizabua Ujerumani mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika kwenye mji wa Marseille Alhamisi iliyopita huku ikijiamini kuilaza Ureno.
Ureno iliingia hatua hiyo baada ya kuzima ndoto za Wales inayonolewa na Chris Coleman. Mechi hiyo ilichezwa kwenye mji wa Lyon.
Endapo Ufaransa itashinda, itakuwa taji lake la kwanza tangu kutwaa ubingwa wa Euro 2000.
Ureno inalitaka taji hilo kwa kuwa haijawahi kulitia mikononi, iliingia fainali na kufungwa na Ugiriki katika Euro 2004 ikiwa nyumbani kwenye mji wa Lisbon.
Gazeti la Michezo la Ufaransa, L’Equipe liliandika vichwa vingi vya habari baada ya Ufaransa kuitoa Ujerumani likiandika; “L’Extase” (Furaha) baadaye “L’Horreur” (Mapinduzi) ikielekeza, mapinduzi ya Novemba 14, mjini Paris.
Vijana wa Didier Deschamps’ wanataka kumaliza kazi mapema lakini wanamuwaza mshambuliaji wa Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo, ambaye alifunga na kutengeneza bao katika mechi dhidi ya Wales.
Kipa wa Ufaransa na Tottenham, Lloris alisema mechi ya fainali ina umuhimu wake: “Mashabiki walitaka kuipuuza michuano hii, lakini nimeona michezo imewaunganisha tena. “Unaweza kuona. Bado tuna kazi moja ya kuvuka mbele, ni ngumu, lakini itapendeza kama tukifanya kitu.”
Antoine Griezmann, anayeongoza kwa mabao, ana matumaini ya kutwaa ubingwa na kiatu cha dhahabu.
Ureno iliingia fainali ya Euro 2004 na kupoteza, pia walipoteza katika nusu fainali Kombe la Dunia 2006, robo fainali ya Euro 2008 na nusu fainali ya Euro 2012.
Pia, iliwahi kupoteza katika nusu fainali dhidi ya England mwaka 1966.
Ufaransa iliingia fainali baada ya kuizabua Ujerumani mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika kwenye mji wa Marseille Alhamisi iliyopita huku ikijiamini kuilaza Ureno.
Ureno iliingia hatua hiyo baada ya kuzima ndoto za Wales inayonolewa na Chris Coleman. Mechi hiyo ilichezwa kwenye mji wa Lyon.
Endapo Ufaransa itashinda, itakuwa taji lake la kwanza tangu kutwaa ubingwa wa Euro 2000.
Ureno inalitaka taji hilo kwa kuwa haijawahi kulitia mikononi, iliingia fainali na kufungwa na Ugiriki katika Euro 2004 ikiwa nyumbani kwenye mji wa Lisbon.
Gazeti la Michezo la Ufaransa, L’Equipe liliandika vichwa vingi vya habari baada ya Ufaransa kuitoa Ujerumani likiandika; “L’Extase” (Furaha) baadaye “L’Horreur” (Mapinduzi) ikielekeza, mapinduzi ya Novemba 14, mjini Paris.
Vijana wa Didier Deschamps’ wanataka kumaliza kazi mapema lakini wanamuwaza mshambuliaji wa Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo, ambaye alifunga na kutengeneza bao katika mechi dhidi ya Wales.
Kipa wa Ufaransa na Tottenham, Lloris alisema mechi ya fainali ina umuhimu wake: “Mashabiki walitaka kuipuuza michuano hii, lakini nimeona michezo imewaunganisha tena. “Unaweza kuona. Bado tuna kazi moja ya kuvuka mbele, ni ngumu, lakini itapendeza kama tukifanya kitu.”
Antoine Griezmann, anayeongoza kwa mabao, ana matumaini ya kutwaa ubingwa na kiatu cha dhahabu.
Ureno
Wachezaji wa Ureno wanataka kuweka rekodi kwani wameikosa kwa muda mrefu, ikiwemo kuingia fainali bila mafanikio.Ureno iliingia fainali ya Euro 2004 na kupoteza, pia walipoteza katika nusu fainali Kombe la Dunia 2006, robo fainali ya Euro 2008 na nusu fainali ya Euro 2012.
Pia, iliwahi kupoteza katika nusu fainali dhidi ya England mwaka 1966.
ZeroDegree.
Fainali ya kombe la EURO 2016 kuchezwa leo; Ufaransa wataka rekodi huku Ureno wakisaka heshima.
Reviewed by Zero Degree
on
7/10/2016 01:06:00 PM
Rating: