Loading...

Gerson Lwenge, awa Rais Baraza la Maji Afrika.

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge, amekabidhiwa kijiti cha urais wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa Nchi za Afrika(AMCOW), ili kuwa kiongozi wa taasisi hiyo kwa miaka miwili.

Wawakilishi kutoka nchi mbalimbali barani Afrika,wakiwa katika mkutanob mkuu wa maazimisho ya wiki ya maji Barani Afrika, uliofanyika jijini Dar es Salaam, jana.

Alikabidhiwa wadhifa huo katika mkutano wa 10 wa baraza hilo ulimalizika jana jijini Dar es Salaam, ambao ulihusisha mawaziri zaidi ya 40 kutoka Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea jukumu hilio alisema atakuwa na kazi kubwa ya kuangalia mikakati ya kila nchi ili kufikia malengo na kuondokana na changamoto mbalimbali zinazoletwa na uhaba wa maji.

Alisema changamoto kubwa inayokwamisha utekelezaji wa malengo ambayo nchi hizo zimejiwekea ili kuwafikishia wananchi wake maji safi na salama ni fedha na kwamba kunahitajika mbinu mbadala kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kutimiza azama hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa AMCOW aliyemaliza muda wake, Bai Maa Staa, alisema changamoto ni miundombinu, hivyo serikali zinatakiwa kuwekeza katika miundomsingi ili kuwapatia wananchi maji badala ya kutembea umbali mrefu.

ZeroDegree.
Gerson Lwenge, awa Rais Baraza la Maji Afrika. Gerson Lwenge, awa Rais Baraza la Maji Afrika. Reviewed by Zero Degree on 7/23/2016 10:56:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.