Loading...

Juma Kaseja ateuliwa kuwa kocha Serengeti boys.

Juma Kaseja.

KIPA wa Mbeya City, Juma Kaseja ameteuliwa kuwa kocha wa makipa wa timu ya Vijana ya soka chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti boys’.


Akizungumza na waandishi wa habari jana Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alisema kuwa Kaseja anachukua nafasi ya kocha Mwarami Mohamed ambaye atakuwa kwenye kozi ya juu ya makipa.

“Serengeti Boys imeondoka leo (jana) kwenda kuweka kambi nchini Madagascar kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa raundi ya pili kuwania kufuzu fainali za mataifa Afrika kwa vijana wa umri huo dhidi ya Afrika Kusini na Kaseja yupo kwenye safari hiyo kama kocha wa makipa,” alisema Lucas.

Pia Lucas alisema kwenye kikosi hicho atakosekana kocha msaidizi Seba Nkoma ambaye yupo kwenye kozi ya makocha ya leseni A.

Serengeti Boys itaweka kambi Madagascar kwa siku kumi kabla ya kuikabili Afrika Kusini Agosti 6 Johannesburg kabla kurudiana Agosti 21 nyumbani.

Endapo Serengeti Boys itafanikiwa kuitoa Afrika Kusini itapambana na timu kati ya Namibia au Congo Brazaville na ikiwa itafanikiwa kushinda itakuwa imefuzu kwenda Madagascar zitakapofanyika fainali hizo mwakani.


Credits: Habari Leo
ZeroDegree.
Juma Kaseja ateuliwa kuwa kocha Serengeti boys. Juma Kaseja ateuliwa kuwa kocha Serengeti boys. Reviewed by Zero Degree on 7/27/2016 11:34:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.