Loading...

Kadi za Magari ya MWENDOKASI sasa kuuzwa shilingi 2000/=.

Meneja uhusiano wa mabasi ya mwendo wa haraka UDART Bwana Deus Bugaiwa amesema wameamua kushusha kwa muda bei ya kadi za kusafiria kwenye mabasi hayo kutoka Shilingi 5000 hadi kufikia shilingi 2000.

Lengo ni kuwafikia watumiaji wengi wa kadi kuzipata na pia kusaidia mfumo ufanye kazi kwa ufanisi kwakua umeandaliwa kwaajili ya matumizi ya kadi na tiketi zitatumika kwa wanafunzi pekee.

Bwana Deus ameyasema hayo wakati akifafanua namna ya Shirika hilo lilivyojipanga katika kuhakikisha linakabiliana na changamoto ambazo zinaweza kujitokeza katika matumizi ya mfumo wa kadi baada ya kusitishwa kwa mfumo wa tiketi mwishoni mwa mwezi huu.

Amesema tayari wameanza kusambaza kadi kwenye vituo vyote na utaratibu huu utasaidia sana kupunguza foleni kwenye vituo hivyo ambavyo kwa sasa kumekua na msongamano wa abiria ambao wanahitaji tiketi badala ya kadi.

Ameongeza utumiaji huo wa kadi utaongeza pato la taifa moja kwa moja na kuongeza ufanisi wa kazi na kupunguza malalamiko kutoka kwa watumiaji ambao wanakua wakikutana na changamoto za tiketi hasa kwenye tatizo la mtandao wa Internet.

ZeroDegree.
Kadi za Magari ya MWENDOKASI sasa kuuzwa shilingi 2000/=. Kadi za Magari ya MWENDOKASI sasa kuuzwa shilingi 2000/=. Reviewed by Zero Degree on 7/26/2016 10:59:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.