Loading...

Kibaki azungumzia tatizo la maji Afrika.

Rais Mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki.

Mwai Kibaki, amesema serikali za nchi za Afrika moja moja hazitafanikiwa kufikia malengo ya maendeleo
iliyojipangia kama hakutakuwapo na ushirikiano wa hali na mali na wa wadau wa maendeleo kusaidia shughuli za maendeleo.

Kibaki alisema hayo jana wakati akizungumza katika mkutano wa sita wa wiki ya maji jijini Dar es Salaam, uliowakutanisha mawaziri, watendaji na wadau wengine wa maji katika nchi za Afrika.

Kati ya mambo ambayo Kibaki alisema yanahitaji ushiriki wa wadau wengine kupiga hatua ni upatikanaji wa maji safi na salama kwani serikali nyingi hazijafanikiwa kuwapatia wananchi wake huduma hiyo.

Alisema pamoja na kuangalia mbinu mbadala ya kutatua tatizo hilo Afrika, lakini pia kuna haja ya kuiwezesha sekta ya maji kwa kuitengea fedha za kutosha na nyenzo za kitaalam ambazo zitasaidia kusambaza maji katika maeneo yote ya mijini na vijijini.

“Tatizo jingine linalosababisha nchi hizo zisifanikiwe kuwapatia wananchi wake huduma ya maji safi na salama ni nchi hizo kutojua namna ya kujipanga na kutumia teknolojia na kutatua tatizo hilo pamoja na kushindwa kutenga fedha za kutosha. Tunahitaji kuangalia mbinu mbadala za kupambana na tatizo hili haraka,” aliongeza.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, aliwataka mawaziri, watendaji, watunga sera, watafiti na wadau wanaokutana katika mkutano huo, kujadili na kuja na majibu ya kutatua tatizo la maji katika nchi hizo kwa kutumia rasilimali zilizopo katika nchi hizo ikiwamo maziwa, mito na vyanzo vingine.


ZeroDegree.
Kibaki azungumzia tatizo la maji Afrika. Kibaki azungumzia tatizo la maji Afrika. Reviewed by Zero Degree on 7/19/2016 11:59:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.