Loading...

Kocha mpya wa Man City Pep Guadiola, amewapiga marufuku wachezaji wake kula PIZZA.

Guardiola amepiga marufuku ulaji wa Pizza baadhi ya sharutabi na vyakula vingine vyenye mafuta mengi.

Kocha mpya wa Manchester City Pep Guardiola amepiga marufuku ulaji wa vyakula vya kupigwa kwa haraka na vile vinavyopikwa kwa mafuta mengi..

Mlinzi wa klabu hiyo Gael Clichy amewaambia waandishi wa habari kuwa mhispania huyo amepiga marufuku vyakula hivyo vya kisasa mbali na kuwafukuza wachezaji walionenepa kutoka kwenye mazoezi ya klabu hicho maarufu cha Manchester .

Clichy amesema kuwa wameharamishwa kula Pizza baadhi ya sharutabi na vyakula vingine vyenye mafuta mengi.

hayo ni katika maandalizi ya mechi ya kufungua msimu huu dhidi ya Sunderland tarehe 13 Agosti.

''endapo umenenepa hutajiunga na timu katika mazoezi''

Ikiwa uzani wako wa kawaida ni takriban kilo 60 na ukapatikana umegonga kilo 70 fahamu kuwa utapigwa marufuku hadi pale utakapopunguza uzani wako.''

Tayari wachezaji kadhaa wamepigwa marufuku kujiunga na kikosi cha timu katika mazoeozi.''


Pep apiga marufuku Pizza Man City

''Kwa kweli hii ndiyo mara ya kwanza kabisa kwa kocha yeyote yule kudhibiti uzani wa wachezaji .''

''Ni jambo la kufurahia, inakupa nadharia ya klabu kinachoendeshwa kitaaluma'' Mchezaji huyo raia wa Ufaransa alielezea.

City watachuana hapo kesho dhidi ya Borussia Dortmund katika mchuano wa kimataifa wa vilabu bingwa unaoandaliwa Shenzhen, China.

Mechi ya kujipima nguvu dhidi ya mahasimu wao katika mji wa Manchester, Red Devils ilitupiliwa mbali baada ya mvua kubwa kunyesha mjini Beijing Uchina.

Credits: BBC Swahili
ZeroDegree.
Kocha mpya wa Man City Pep Guadiola, amewapiga marufuku wachezaji wake kula PIZZA. Kocha mpya wa Man City Pep Guadiola, amewapiga marufuku wachezaji wake kula PIZZA. Reviewed by Zero Degree on 7/28/2016 12:12:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.