Loading...

Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu [ AfCHPR ], yasitisha hukumu ya kifo


Jaji Agustino Ramadhani, Rais AfCHPR.

Arusha. Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu (AfCHPR) imeitaka Serikali ya Tanzania kutokutekeleza hukumu ya kunyongwa hadi kufa iliyotolewa na Mahakama ya Rufaa nchini dhidi ya Amini Juma hadi maombi aliyoyawasilisha katika mahakama hiyo yatakapotolewa uamuzi.

Pia mahakama hiyo ya Afrika imeitaka Serikali kutoa taarifa za utekelezaji wa maagizo yake ndani ya siku 60 baada ya kupokea taarifa rasmi za AfCHPR. 

Amini ambaye kwa sasa anashikiliwa kwenye gereza la Maweni mkoani Tanga, alihukumiwa kutumikia kifungo cha maisha gerezani na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Septemba 18, 2008 baada ya kutiwa hatiani kwa mauaji yaliyofanyika eneo la Meserani wilayani Monduli mkoa wa Arusha.
Hata hivyo alikata rufaa kupinga hukumu hiyo lakini Mahakama ya Rufaa iliitupilia mbali hukumu hiyo na kuamuru mtuhumiwa anyongwe hadi kifo.

Amini anadai baada ya hukumu ya Mahakama ya Rufaa alitoa maombi ya kupitiwa upya hukumu hiyo, lakini Mahakama imechelewesha kufanya hivyo hadi alipowasilisha maombi yake AfCHPR Aprili katika kesi iliyopewa namba 024/2016.

Katika maelezo yake AfCHPR anadai kuwa ushahidi uliowasilishwa katika Mahakama Kuu na upande wa mashtaka ulikuwa na maelezo yasiyojitosheleza kumtia hatiani.


Zerodegree.
Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu [ AfCHPR ], yasitisha hukumu ya kifo Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu [ AfCHPR ], yasitisha hukumu ya kifo Reviewed by Zero Degree on 7/04/2016 01:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.