Mahakama yakanusha taarifa ya gazeti la Mwananchi.
Mahakama ya Tanzania imetoa taarifa ya kutoa ufafanuzi kwa umma juu ya habari iliyoandikwa na gazeti la kila siku la Mwananchi toleo la Jumanne, Julai 12, 2016.
Gazeti hilo lilichapisha habari ambayo Mwandishi wa habari hiyo alimnukuu Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Katarina Revokati akiwataka watendaji wa mahakama nchini kujenga utamaduni wa kuwajibika na kutoruhusu uhuru wa mahakama kuingiliwa na watu kutoka nje ya Mahakama.
Kutokana na habari hiyo, Mahakama ya Tanzania imekanusha taarifa hiyo kwa kuwa ililenga katika kuipotosha jamii na kuleta msuguano kati ya Mahakama na Taasisi nyingine.
Mahakama imetoa ufafanuzi na kueleza kuwa, Mahakama ya Tanzania inapenda kutoa ufafanuzi wa alichokisema Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania wakati wa ufunguzi wa Mkutano kuhusu Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania Jumatatu Julai 11, 2016 mjini Dodoma.
Aidha, Msajili aliwataka watumishi wa mahakama nchini kutekeleza mpango mkakati kwa nia thabiti na siyo kuutumia uhuru wa mahakama vibaya kufunika maovu, badala yake aliwataka wale wenye kasoro katika utendaji wa kazi kujirekebisha wao wenyewe ndani ya mahakama la sivyo watarekebishwa hata kutokea nje kwani jamii yetu kwa sasa imedhamiria kubadilika na haitavumilia utendaji mbovu kwa kigezo cha uhuru wa mahakama.
Taarifa ya Mahakama ya Tanzania imeeleza kuwa mahakama inapenda kuujulisha umma kuwa inafanya kazi na watu wote na wadau wote nchini ili kuhakikisha nchi inaenda inavyotakiwa na haitaogopa kukosolewa kinyume na picha iliyopelekwa kwa jamii na habari iliyopotoshwa kwenye gazeti la Mwananchi.
Aidha mahakama inashauri waandishi wa habari kuwasiliana na Mahakama endapo kuna jambo lolote linalohitaji ufafanuzi. Makosa mengine katika taarifa ni kama vile kukosea cheo kwa kusema Jaji badala ya Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na kuandika taarifa kuhusu hatua zinazochuliwa kwa Wahe. Majaji waliohusika na sakata la ESCROW ambapo kiukweli katika mkutano huu halikuongelewa kabisa.

ZeroDegree.
Mahakama yakanusha taarifa ya gazeti la Mwananchi.
Reviewed by Zero Degree
on
7/14/2016 10:56:00 AM
Rating: