Loading...

Mbeya City kuja kivingine.

KOCHA wa Mbeya City, Kinnah Phiri alisema anaamini msimu ujao utakuwa bora zaidi kwa timu yake kutokana na maandalizi aliyoyaanza.

Phiri alisema tayari ameshaielewa ligi ya Tanzania na msimu ujao hakutakuwa na jambo geni kwake.

"Maandalizi yetu yanaendelea vizuri. Upungufu tuliokuwa nao msimu uliopita, ndiyo tunaoufanyia kazi kwa sasa," alisema Phiri.

Kocha huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Malawi, alisema anaamini wachezaji watakaoongezwa kwenye kikosi chake watakuwa na msaada mkubwa kwake.

"Nataka msimu ujao tupige hatua, tutoke pale tulipokuwa msimu uliomalizika," alisema Phiri.

Kikosi cha Mbeya City kimeweka kambi mjini Kyera kujiandaa na ligi kuu iliyopangwa kuanza Agosti 20.


ZeroDegree.
Mbeya City kuja kivingine. Mbeya City kuja kivingine. Reviewed by Zero Degree on 7/20/2016 10:27:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.