Mbio zamkimbiza Boban Mbeya City.
KOCHA wa Mbeya City, Kinnah Phiri amejificha katika ufukwe wa Matema wilayani Kyela akiwapa wachezaji wake mbinu mpya za ushindi katika mechi za ligi kuu msimu ujao huku akiweka wazi kuwa kiungo wake mahiri, Haruna Moshi ‘Boban’ ameshindwa kuendelea naye kwani anachokihitaji sasa ni wachezaji wenye kasi ya kukimbia.
Akizungumza na Mwanaspoti, Phiri alisema soka la sasa linahitaji wachezaji vijana wanaoweza kukimbia bila kuchoka tofauti na kiungo huyo ambaye msimu uliopita aliisaidia timu hiyo kutoshuka daraja lakini kasi yake ya kukimbia imeelezwa kuwa ilikuwa ndogo.
“Nimeamua kuweka kambi huku kwani hali ya hewa ni ya joto tofauti na Mbeya mjini ambako baridi kali mno, mechi zetu tatu za mwanzo tutaanzia ugenini hivyo lazima wachezaji wawekwe sehemu ambayo hali ya hewa itaendana na mnakokwenda lakini pia kuna utulivu, ratiba hii imekaa vizuri, tutacheza mechi zote sehemu moja ndipo tutarudi nyumbani tofauti na ile ya msimu uliopita.
“Boban ni mchezaji mzuri lakini nimeona vyema nisajili vijana wengi wenye kasi kubwa ya kukimbia bila hiyo unaweza kufeli, kikosi changu msimu ujao hakitatetereka kwani nimesajili mwenyewe na wengine niliwakuta ambao nawafahamu vizuri,” alisema.
Kwa nafasi zilizoboreshwa Phiri alisema: “Ukiangalia nafasi ya ulinzi ipo vizuri, viungo wapo wengi lakini hata washambuliaji, hivyo nitakuwa na uwezo wa kuchagua nitakavyo, naamini pia Juma Kaseja hataniangusha maana tunamsubiri kama alivyotuahidi, atasaidiana na kipa wa Big Bullets, Owen Chaima anayetarajia kutua leo (jana). “Straika Chiukepo Msowoya hatakuja, kuna vijana wanaoiweza kazi kama yake, lazima wazawa wapewe nafasi, yupo Mohamed Mkopi na Omary aliyetoka African Sports,” alisema Phiri.

Reviewed by Zero Degree
on
7/26/2016 11:44:00 AM
Rating: