Loading...

Mgombea Urais nchini Marekani [ Chama cha Republican ], Donald Trump awakumbuka Saddam Hussein na Gaddafi.

Donald Trump amemsifu kiongozi wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein akisema aliweza kukabiliana vyema na magaidi.


Trump alikuwa akihutubia mkutano wa kampeni eneo jimbo la North Carolina na kuanza kuzungumza kuhusu kiongozi huyo aliyeuawa kwa kunyongwa Desemba 2006.

“Saddam alikuwa mbaya, kweli? Lakini mnafahamu ni jambo gani aliweza kulifanya vyema? Aliwaua magaidi,” alisema Trump. 

Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump.  
Trump aliwahi kusema kwamba ulimwengu ungelikua salama zaidi kuliko sasa iwapo viongozi kama Saddam Hussein na kiongozi wa muda mrefu wa Libya Muammar Gaddafi wangelikuwa madarakani.

Kabla ya uvamizi ulioongozwa na Marekani, Saddam aliondolewa madarakani, Iraq ilikuwa imeorodheshwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kama taifa linalofadhili magaidi.

Mshauri mkuu wa Hillary Clinton kuhusu sera, alijibu matamshi ya Trump kwa kusema kuwa “Sifa za Trump kwa viongozi hazina mipaka.”

Alisema matamshi kama hayo yanaashiria ni jinsi gani itakuwa hatari (kuwa na Trump) kuwa Amiri Jeshi Mkuu na ambavyo hafai kutumikia kama rais.

Trump alisema maafa yanayoendelea Mashariki ya Kati yalichangiwa asilimia mia moja na sera mbovu za Rais Obama na Hillary Clinton.

‘’Japo tunamlaumu Muammar Gaddafi unadhani angekuwa hai magaidi wangekuwa huko? Libya tuliyoijua sasa imesambaratika kabisa, ’’alisema Trump.

Aliongeza, “Saddam alikuwa mtawala, asingeliwaruhusu magaidi kufurukuta Iraq. Sasa Iraq ndiyo Havard ama chuo kikuu zaidi cha ugaidi duniani.”alisema Trump

Trump alisema anaamini kabisa kwamba yeye ataongoza nchi hiyo kwa sababu anazo sifa zote za kutawala Marekani.


Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Mgombea Urais nchini Marekani [ Chama cha Republican ], Donald Trump awakumbuka Saddam Hussein na Gaddafi. Mgombea Urais nchini Marekani [ Chama cha Republican ], Donald Trump awakumbuka Saddam Hussein na Gaddafi. Reviewed by Zero Degree on 7/07/2016 12:22:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.