Loading...

Mjomba Kundambanda kuzikwa leo.

Aliyekuwa Mchekeshaji maarufu kutoka kundi la Vituko Show, Ismail Makombe maarufu kama Baba/Mjomba Kundambanda wakati wa uhai wake.

Mchekeshaji maarufu kutoka kundi la Vituko Show, Ismail Makombe maarufu Baba Kundambanda, aliyefariki dunia jana atazikwa leo saa kumi jioni nyumbani kwao Masasi mkoani Mtwara. 


Pia, Kundambanda aliyekuwa mwanasiasa aligombea ubunge wa Jimbo la Masasi mkoani Mtwara kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) katika Uchaguzi Mkuu 2015.

Naibu Katibu mkuu wa CUF Tanzania Bara, Shaweji Mketo alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kwamba, Kundambanda ameacha pengo kubwa kwao.

Wakati wa uhai wake, Kundambanda pia, alikuwa mtunzi wa nyimbo za kuhamasisha harakati mbalimbali za jamii.




ZeroDegree.
Mjomba Kundambanda kuzikwa leo. Mjomba Kundambanda kuzikwa leo. Reviewed by Zero Degree on 7/23/2016 12:28:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.