Loading...

Mkude asema hana hofu ya namba katika kikosi cha Klabu ya Simba msimu ujao [ Simba inatarajiwa kuweka kambi Lushoto ].

Kiungo Jonas Mkude.

Dar es Salam. Wakati uongozi wa Simba ukiweka wazi kambi ya timu hiyo kufanyika Lushoto, kiungo Jonas Mkude amesema hahofii ushindani wa namba katika kikosi chao msimu ujao kwani anajiamini.

Mkude alisema ushindani wa namba ndiyo huleta changamoto na kuipa mafanikio timu yoyote duniani kwani kila mmoja atajituma ili kupata nafasi kikosi cha kwanza.

Alisema ujio wa viungo wapya waliosajiliwa hivi karibuni katika kikosi hicho wala haumpi presha kwani anajiamini kuwa ana kiwango bora na atajituma kuhakikisha anaendela kuwapo katika kikosi cha kwanza cha kocha Joseph Omog.

Simba imewasajili viungo Mohammed Ibrahim pamoja na Mudhamiru Yassin kutoka Mtibwa Sugar, hivyo kufanya idadi ya viungo kuwa nane wakiwamo Mkude, Mwinyi Kazimoto, Said Ndemla, Peter Mwalyanzi, Awadhi Juma na Justice Majabvi.

“Nawakaribisha viungo wapya waliosajiliwa ili kuendeleza gurudumu la timu yetu, popote kunapokuwa na changamoto ya ushindani wa namba ndipo mafanikio yanakuja kwani kila mmoja anapambana kuhakikisha anacheza ili kuisaidia timu.

“Sina hofu hata kidogo kwani najiamini uwezo wangu na mwisho wa siku kocha ndiye ataamua nani aanze kikosi cha kwanza, lakini malengo ni kuhakikisha tunaisaidia timu kufanya vizuri msimu ujao,” alisema Mkude.

Simba kambini Lushoto


Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuweka kambi Lushoto mkoani Tanga, kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza Agosti.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hanspoppe alisema kambi ya timu hiyo itaanza baada ya Sikuku ya Eid El Fitr, huku akisisitiza kuwa wachezaji wanatakiwa kuwa tayari.

“Tupo ‘serious’ na hatuna utani kwa hili, lazima wajue kuwa wamesajiliwa kwa ajili ya kufanya kazi na siyo vinginevyo. Simba ni timu kubwa yenye mashabiki ndani na nje ya nchi, hatutaki kuona tunakwama msimu huu,” alisema Hanspoppe.

Alisema baada ya kambi hiyo, wataanza kucheza mechi dhidi ya timu za daraja la nne, tatu, pili na la kwanza kabla ya kuanza kucheza mechi za kujipa nguvu za kimataifa.

“Mtazamo wetu ni timu za Rwanda, hii inatokana na ukweli kuwa kuna timu ngumu, tukishindwa basi itakuwa timu za Kenya na Uganda, tunataka kuona jinsi gani tunafikia lengo letu.


ZeroDegree.
Mkude asema hana hofu ya namba katika kikosi cha Klabu ya Simba msimu ujao [ Simba inatarajiwa kuweka kambi Lushoto ]. Mkude asema hana hofu ya namba katika kikosi cha Klabu ya Simba msimu ujao [ Simba inatarajiwa kuweka kambi Lushoto ]. Reviewed by Zero Degree on 7/05/2016 12:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.