Loading...

Mourinho mwamuzi wa nafasi ya Rooney Uingereza.

Wayne Rooney

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho ataamua ni safu gani ambayo Wayne Rooney atalichezea taifa lake ,kulingana na mkufunzi mpya wa Uingereza Sam Allardyce.


Rooney mwenye umri wa miaka 30 alicheza safu ya mashambulizi chini ya mkufunzi Roy Hodgson katika michuano ya Euro 2016.

Mkufunzi mpya wa Uingereza Sam Allardyce

Lakini Allardyce amesema kuwa ni mapema mno kuthibitisha iwapo Rooney,ambaye analiongoza taifa lake katika ufungaji wa mabao atasalia kuwa nahoda wa timu hiyo.

''Nadhani Wayne Rooney bado ana fursa kubwa kuchezea Uingereza'', alisema mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 61.


Kocha wa Manchester United Jose Mourinho.

''Iwapo Jose atasema kwamba hatamchezesha katika safu ya kati na anamchezesha katika eneo la mashambulizi katika klabu ya Manchester United,itakuwa haina maana yoyote mimi kumchezsha katika safu ya kati''.

ZeroDegree.
Mourinho mwamuzi wa nafasi ya Rooney Uingereza. Mourinho mwamuzi wa nafasi ya Rooney Uingereza. Reviewed by Zero Degree on 7/27/2016 12:07:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.