Loading...

Cannavaro awatoa presha mashabiki juu ya hatima yao katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Nadir Haroub ‘Cannavaro’ 

Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema bado wana michezo minne ya kuamua hatima yao katika mashindano Kombe la Shirikisho Afrika na kuwataka mashabiki wao wapunguze presha.


Yanga imepoteza michezo miwili wakifungwa ugenini na nyumbani dhidi ya MO Bejaia na TP Mazembe kwa bao 1-0.

Jambo hilo limeanza kuwatia wasiwasi wadau mbalimbali wa soka wanaoamini safari ya Yanga inaelekea kubaya ikiwa inakamata mkia katika Kundi A.

Nahodha Cannavaro alisema Yanga haiwezi kuwa ya mwisho katika kundi lao kwani watapambana kuhakikisha michezo minne iliyobaki wanashinda yote.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara watashuka tena uwanjani kati ya Julai 15 na 17 kwenye Uwanja wa Taifa, Da es Salaam, kuikaribisha Medeama ya Ghana.

“Baada ya kupoteza michezo miwili, wengi wameanza kukata tamaa na kuona hatuwezi kufanya vizuri katika michezo iliyobaki, lakini wanajidanganya.

“Tuna michezo minne imebaki, miwili nyumbani na miwili ugenini, tuna uwezo wa kushinda yote kama tutajiandaa vizuri, bado kikosi chetu ni kizuri na kina nguvu ya kupambana katika michezo hiyo na kupata ushindi,” alisisitiza Cannavaro.

Cannavaro ambaye amepoteza namba yake katika kikosi cha kwanza tangu aliporejea kutoka katika majeruhi aliongeza kuwa:

“Muhimu ni kujiongeza katika michezo ijayo na kujua wapi tulikosea katika michezo iliyopita.

“Wachezaji tuna ari ya kuendelea kupambana na kuhakikisha tunamaliza tukiwa wa kwanza katika kundi letu, hiyo inawezekana kwani huwezi kujua wapinzani wetu wanaoongoza kundi sasa, matokeo ya mechi zijazo yatakuaje, hivyo lolote linaweza kutokea.”





ZeroDegree.
Cannavaro awatoa presha mashabiki juu ya hatima yao katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika. Cannavaro awatoa presha mashabiki juu ya hatima yao katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika. Reviewed by Zero Degree on 7/05/2016 12:42:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.