Loading...

Polisi wakiri kosa kiutendaji.

Dodoma. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amekiri kutokea kwa makosa wakati wa uandaaji wa hati ya mashtaka dhidi ya viongozi wanne wa Taifa wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha).

Wanaoshikiliwa ni Mwenyekiti wa Taifa, Patrobas Katambi, Katibu Mkuu, Julius Mwita, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Joseph Kasambala na Mwenyekiti wa Mkoa wa Mbeya, George Tito.

“Mahojiano yameisha, charge sheet (hati ya mashtaka) ikaandaliwa, lakini ikarudishwa tuifanyie marekebisho. Muda umepita wa Mahakama” amesema .

Hata hivyo, amesema kesi hiyo haina dhamana kwa upande wa kituo cha polisi na hivyo kuwalazimu watuhumiwa hao kuendelea kukaa rumande.

Wakili wa watuhumiwa hao, Fred Kalonga amesema wamekuwa na wateja wao tangu siku walipokamatwa kwa kuhakikisha wanahojiwa kwa mujibu wa sheria.

Amesema yeye na wakili mwenzake, Azack Mwaipopo walikuwa wanakwenda kufuatilia taratibu nyingine za kisheria za kuwawezesha kupata dhamana.

“Tunakwenda kufuatilia taratibu nyingine lakini sisi tupo tayari muda wowote wakiletwa tutawa-defend (tutawatetea) kwasababu tunaamini kwa mujibu wa maelezo ya wateja wetu wapo sahihi kuliko tuhuma zinazowakabili,” alisema.


Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Polisi wakiri kosa kiutendaji. Polisi wakiri kosa kiutendaji. Reviewed by Zero Degree on 7/12/2016 09:52:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.