Loading...

Spika wa Bunge, Job Ndugai anatarajiwa kurejea nchini hivi karibuni.

Spika wa Bunge, Job Ndugai

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge, Owen Mwandumbya amesema
Spika wa Bunge, Job Ndugai anatarajiwa kurejea nchini kutoka India ambako anatibiwa kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Akizungumza kwa simu na gazeti hili jana, Mwandumbya alisema Spika huyo anaendelea vizuri na anatarajiwa kurejea nchini hivi karibuni.

Mara ya mwisho Ndugai kuonekana bungeni, ilikuwa wiki ya pili baada ya kikao cha tatu cha Bunge la 11 kuanza, Aprili 19.

Hadi Bunge la 11, lililojadili na kupitisha bajeti kwa mwaka wa fedha 2016/17 na kuahirisha vikao vyake mapema Julai, vikao vyote vilikuwa vikiongozwa na Naibu Spika Dk Tulia Ackson.



Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Spika wa Bunge, Job Ndugai anatarajiwa kurejea nchini hivi karibuni. Spika wa Bunge, Job Ndugai anatarajiwa kurejea nchini hivi karibuni. Reviewed by Zero Degree on 7/22/2016 03:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.