Siku ya Mashujaa kuadhimishwa kwa kufanya usafi.
Ni jambo jema kwa Taifa kuwakumbuka kwa kutambua mchano wa wale waliopambana kwa ajili ya Taifa hili, ambapo matunda yaliyopatikana leo yanatokana na wao hivyo, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Dodoma na kimkoa yatafanyika dar-es-salaam siku ya tarehe 25 katika viwanja vya Mnazi mmoja .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwa niaba ya mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amesema kuwa maadhimisho hayo ni kumbukumbu muhimu nchini kwani hiyo ni ishara ya kuwaenzi mashujaa waliojitoa muhanga katika jitihada za kuikomboa Tanzania,kwa kulinda na kudumisha amani nchini.
Hivyo katika maadhimisho hayo kutakuwa na shughuli za uwekaji wa silaha za asili na maua kwenye mnara wa kumbukumbu wa uhuru,gwaride la maadhimisho ya kumbukumbu litakaloandaliwa na vikosi vyaa JWTZ, Polisi Magereza pamoja na JKT.

Mkuu wa wilaya ya Ilala Mjema ameongeza kuwa serikali inatoa wito kwa makampuni, mashirika, taasisi pamoja na wakazi wa maeneo ya Mnazi Mmoja kufanya usafi katika maeneo yao ili kuipa nguvu siku hiyo adhimu ya mashujaa na kuwataka watanzania kujitokeza kwa wingi.
Source: Mtembezi
ZeroDegree.
Siku ya Mashujaa kuadhimishwa kwa kufanya usafi.
Reviewed by Zero Degree
on
7/22/2016 03:34:00 PM
Rating: