Loading...

Tetesi za usajili Barani Ulaya leo siku ya Jumanne.

Harry Kane atasaini mkataba mpya kusalia White Hart Lane, Kiungo wa Paris St-Germain, Blaise Matuidi, 29, amepewa ruhusa ya kuondoka kambi ya Ufaransa Euro 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuhamia Manchester. Pogba kurejea OT..??


Kane kupatiwa mkataba mnono.

Mshambuliaji wa England na Tottenham, Harry Kane atasaini mkataba mpya kusalia White Hart Lane wenye thamani ya pauni milioni 5 kwa mwaka wiki hii (Independent), Jose Mourinho ana uhakika wa kumshawishi kiungo kutoka Ufaransa Paul Pogba, 23, kurejea tena Manchester United miaka minne baada ya kuondoka na kwenda Juventus (Daily Mail), Manchester United wapo tayari 'kuvunja benki' ili kumsajili Pogba, huku dau likidhaniwa kufika hadi pauni milioni 100 (Telegraph).

Pogba kurejea OT?

Kiungo wa Paris St-Germain, Blaise Matuidi, 29, amepewa ruhusa ya kuondoka katika kambi ya Euro 2016 ya Ufaransa na kwenda England kwa ajili ya mazungumzo ya kuhamia Manchester United, Manchester United na Liverpool wote wanataka kumsajili kiungo wa Porto Ruben Neves, 19 (Sun), Manchester City wanakaribia kukamilisha usajili mwingine unaodhaniwa kuwa wa pauni milioni 40 kumchukua winga wa Schalke, Leroy Sane, 20 (Manchester Evening News), Tottenham hatimaye wanakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa AZ Alkmaar, Vincent Janssen, 21, wiki hii na pia wanataka kumsajili mshambuliaji wa Roma, Antonio Sababria, 20 na Lucas Alario, 20 kutoka River Plate (Daily Mirror).

Alvaro Morata anasakwa na vilabu kadhaa vya EPL

Arsenal wako tayari kumpa Alvaro Morata, 23, mshahara wa pauni 144,000 kwa wiki kumshawishi kuhamia Emirates (Don Balon), Crystal Palace wameongeza dau lao kufikia pauni milioni 31.5 kumtaka mshambuliaji wa Liverpool Christian Benteke, 25, baada ya dau la pauni milioni 25 kukataliwa (Sun), Crystal Palace wanakamilisha uhamisho wa beki wa West Ham James Tomkins, 27 (Evening Standard), Chelsea wanafikiria kutoa pauni milioni 12 kumchukua mshambuliaji wa Southampton Graziano Pelle, 30, iwapo watashindwa kumpata Morata kutoka Real Madrid (Evening Standard).

Robin van Persie huenda akarejea London

Kiungo wa Liverpool Lucas Leiva, 29, yuko tayari kuhamia Besitkas ya Uturuki (Fanatik), Fernabahce wanataka kumsajili mshambuliaji wa Newcastle Siem de Jong, 27 (Haberturk), West Ham na Crystal Palace ni miongoni mwa timu za EPL ambazo Robin van Persie, 32, ameruhusiwa kwenda na klabu yake ya Fernabahce (Daily Mail), mshambuliaji wa zamani wa Aston Villa Charles N'Zogbia, 29, anajaribu kufufua mpira wake kwa kufanya mazoezi na Sunderland (Birmingham Mail). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.


Source: BBC
ZeroDegree.
Tetesi za usajili Barani Ulaya leo siku ya Jumanne. Tetesi za usajili Barani Ulaya leo siku ya Jumanne. Reviewed by Zero Degree on 7/05/2016 11:14:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.