Loading...

VIDEO: Materazzi aweka wazi kilichomfanya apigwe na Zidane miaka 10 iliyopita katika fainali za Kombe la dunia 2006.



Beki wa kati wa zamani wa timu ya taifa ya Italia na klabu ya Inter Milan ya Italia Marco Materazzi, usiku wa July 8 2016 ameamua kuweka wazi kilichomfanya apigwe na nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa ambaye kwa sasa ni kocha wa Real Madrid Zidane.



Marco Materazzi ameweka wazi kilichomfanya Zidane ampige kichwa katika mchezo wa fainali ya Kombe la dunia 2006, tofauti na ilivyokuwa inaripotiwa na wengi, Materraziamekuwa akiombwa na vyombo mbalimbali vya habari duniani lakini alikuwa akikwepa kuzungumzia suala hilo.

“Toka 2006 nimekuwa nikipokea maombi mengi ya kufanya interview, nimeamua kutoa kitabu kinachoeleza ukweli kwa sababu kila mtu anauliza ni nini nilimwambia Zidane hadi akapandwa na hasira na kunipiga kichwa, ni kweli maneno yangu yalikuwa ya kijinga lakini Zidane hakustahili kureact vile”

“Nimekuwa nikisikia vitu vingi kutoka katika miji jirani ya Rome, Naples, Turin, Milan Paris ila mimi nilimtusi kuhusu dada na sio mama yake kama nilivyosoma katika magazeti mengi, mama yangu alifariki nikiwa mdogo, hivyo nisingeweza kumtukania mama yake”






ZeroDegree.
VIDEO: Materazzi aweka wazi kilichomfanya apigwe na Zidane miaka 10 iliyopita katika fainali za Kombe la dunia 2006. VIDEO: Materazzi aweka wazi kilichomfanya apigwe na Zidane miaka 10 iliyopita katika fainali za Kombe la dunia 2006. Reviewed by Zero Degree on 7/09/2016 10:41:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.