Loading...

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa APIGA MARUFUKU uvutaji wa Shisha.


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza viongozi wa dini, wazazi na viongozi wa serikali kupiga marufuku matumizi ya vilevi aina ya shisha kwamba kinawaingiza vijana kwenye majaribu na kuharibu maadili kwenye jamii.

Amesema tamko lililotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda sio kutoka kichwani mwake, bali ni agizo la serikali na kwamba viongozi wote wa mikoa na wilaya na mameya wanatakiwa kukemea suala hilo.

Alisema hayo Dar es Salaam juzi katika futari iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislamu ya Shia Ithna-Asheri, iliyofanyika kwenye msikiti uliopo Mtaa wa Indira Gandhi, iliyokutanisha viongozi mbalimbali wa dini na serikali.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema watakaokaidi agizo hilo pamoja na wauzaji wa vilevi hivyo, watachukuliwa adhabu kali kwa kuwa wazazi na serikali kwa ujumla wana uwezo wa kudhibiti tatizo hilo.

Alisema viongozi wengine wanatakiwa kuunga mkono tamko hilo na kusisitiza kwamba shisha inaharibu nguvu kazi ya Taifa, kwa kuwa inaondoa vijana wenye uwezo kimwili na kiakili ambao wanaweza kufanya kazi. “Nimeambiwa nitoe tamko kama serikali juu ya matumizi ya tumbaku inayoitwa shisha.

Hii ina mchanganyiko mwingi ambao huvutwa na kutoa moshi mwingi, maji yake huwekwa gongo na vilevi mbalimbali hivyo mvutaji hupata ladha mbalimbali ambazo siku akikosa hutafuta mahali popote,’’ alisema Majaliwa.

Alisisitiza kuwa viongozi wa dini wanatakiwa kutumia nyumba za ibada, kukemea matendo hayo ambayo yanasababisha kufanyika kwa uovu pamoja na kuharibu maadili katika jamii.



ZeroDegree.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa APIGA MARUFUKU uvutaji wa Shisha. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa APIGA MARUFUKU uvutaji wa Shisha. Reviewed by Zero Degree on 7/05/2016 10:27:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.