Loading...

Waziri mkuu Kassim Majaliwa, kuwa mgeni rasmi Nanenane.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya wakulima Nanenane ya Kanda ya Mashariki viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo mkoani Morogoro.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen, alisema hayo juzi mjini hapa kuwa Waziri Mkuu atafungua maonesho hayo Agosti mosi, mwaka huu ambayo yanashirikisha halmashauri za wilaya za mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, Tanga na Morogoro.

“Maandalizi ya vipando vya mazao ya aina mbalimbali yamekamilika na bidhaa za kilimo na mifugo kwenye mabanda ya kila halmashauri na mwaka huu pia tuna baadhi ya nchi za nje zimeonesha nia ya kushirikiana nasi kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere,”alisema.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa huyo alisema Waziri Mkuu pia atapata fursa ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha sukari cha Mtibwa ili kujionea shughuli wanazozifanya.

Wakati huo huo, Dk Kebwe alisema mkoa huo upo mbioni kufanya kongamano la uwekezaji Septemba mwaka huu ambalo litashirikisha wadau mbalimbali wa uwekezaji ndani ya mkoa na kuwaomba waandishi wa habari wa mkoa huo kutumia vyema kalamu zao kwa ajili ya kuijenga jamii ya mkoa huo na watanzania wote kwa ujumla.

ZeroDegree.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa, kuwa mgeni rasmi Nanenane. Waziri mkuu Kassim Majaliwa, kuwa mgeni rasmi Nanenane. Reviewed by Zero Degree on 7/30/2016 08:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.