Loading...

Arsenal mbioni kumsajili beki wa klabu ya Valencia, Shkodran Mustafi.

Shkodran Mustafi.
Arsenal inatarajia kukamilisha usajili wa Pauni 30 milioni wa beki wa kati wa Valencia, Shkodran Mustafi saa 24 zijazo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani inasemekana amekubali mkataba wa miaka mitano utakaomfanya alipwe Pauni 75,000 kwa wiki na sasa anasubiri kuitwa kwa vipimo vya afya.

Klabu hizo mbili hadi juzi zilikuwa bado hazijakubaliana juu ya uhamisho huo, lakini inadaiwa kuwa mchakato umefikia katika hatua nzuri.

Mustafi ana mkataba wenye thamani ya Pauni 42 milioni, lakini Valencia wameiambia Arsenal watakubali kitita cha Pauni 30 milioni.

Gunners walionyesha ugumu wa kutoa kitita hicho lakini kwa sasa wapo katika wakati mgumu wa kuziba mapengo ya safu yao ya ulinzi.

Arsenal hadi sasa haina beki wa kati wa kueleweka kutokana na kuwa majeruhi, Per Mertesacker na Gabriel wakiumia wakati wa mechi za maandalizi ya msiomu mpya.


ZeroDegree.
Arsenal mbioni kumsajili beki wa klabu ya Valencia, Shkodran Mustafi. Arsenal mbioni kumsajili beki wa klabu ya Valencia, Shkodran Mustafi. Reviewed by Zero Degree on 8/13/2016 10:43:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.