Paul Pogba afungiwa England.
KIUNGO Paul Pogba wa Manchester United atachelewa kwa wiki moja kuitumikia klabu yake hiyo kwa kuukosa mchezo wa kesho wa ligi kuu dhidi ya Bournemouth baada ya Chama cha soka England (FA) kumsimamisha mchezo mmoja.
Mchezaji huyo aliyeigharimu United pauni milioni 89 ataukosa mchezo huo kutokana na kuwa na kadi mbili za njano alizozipata wakati akiichezea Juventus kwenye mashindano ya Copa Italia.
Pogba ni miongoni mwa wachezaji wanne ambao hawatacheza michezo ya ufunguzi ya ligi kuu kutokana na kuwa na adhabu.
FA ilitumia mtandao wake kuelezea hatua hiyo baada ya kuonekana kuwa na kadi mbili za njano alizozipata akiitumikia michezo ya mwisho klabu yake hiyo ya zamani.
Kanuni za Shiriksiho la soka Ulaya (EUFA) linavitaka vyama vya soka wanachama kufuata kanuni hizo za adhabu ambapo licha ya Pogba kuhama kutoka Italia bado ataitumikia adhabu hiyo akiwa England kwenye klabu yake hiyo aliyojiunga nayo baada ya kuachana nayo zaidi ya miaka minne.
Mchezo wake wa kwanza sasa unatagemewa kuwa dhidi ya Southampton utakaochezwa nyumbani Old Trafford Ijumaa ijayo.

ZeroDegree.
Paul Pogba afungiwa England.
Reviewed by Zero Degree
on
8/13/2016 10:39:00 AM
Rating: