Huu ni mtihani kwa Yanga.
Waswahili husema, maji ukiyavulia nguo huna budi kuyaoga! usemi huo utadhihrika kwa Yanga inapoikaribisha MO Bejaia ya Algeria huku ikitaka kulipa kisasi, pia kutunza heshima.
Yanga iliyofungwa bao 1-0 katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi A uliofanyika usiku saa 6.00 mjini Mouloudia, Algeria, ina kila sababu ya kuifunga MO Bejaia ili kutuliza mizuka ya mashabiki.
Timu hiyo imekuwa ikifungwa mabao kipindi cha kwanza, ikiwa imesaliwa na mechi muhimu ya leo ambayo kama ingekuwa maji, basi ndilo tone la mwisho la kukata kiu. Mchezo huo wa raundi ya tano wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF), matokeo yoyote kwa Yanga yatatosha kuichafulia au kuituliza.
Ikiwa na pointi moja, inashika mkia kwenye kundi hilo, hivyo ushindi leo utaiwezesha kufufua matumaini ya kuungana na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ili kucheza nusu fainali ya mashindano hayo ya pili kwa ukubwa Afrika.
Kimahesabu, Yanga ikipoteza itaaga mashindano kwani hata ikiibuka na ushindi kwenye mechi ya mwisho dhidi ya Mazembe, itafikisha pointi nne ambazo tayari zimepitwa nao, MO Bejaia na Medeama ya Ghana. Pia, matokeo ya sare ya aina yoyote yatamaanisha kufika mwisho wa safari ya mabalozi hao wa Tanzania katika soka kimataifa.

Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Huu ni mtihani kwa Yanga.
Reviewed by Zero Degree
on
8/13/2016 10:36:00 AM
Rating: