Loading...

AUDIO: Majibu ya Lema kwa Waziri Mwigulu kuhusu maandamano ya Septemba 1.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba hivi karibuni akiwa ziarani mkoani Mtwara alizungumza na Askari wa Jeshi la Magereza Mkoani humo na kusema kuwa CHADEMA wasithubutu kuandamana kwani kwa kufanya hivyo si kuwa watakuwa wanatingisha kiberiti cha njiti, bali watakuwa wanachezea gesi. Amesema kuwa sio kila kitu mtu anatakiwa kujaribu kwa sababu vingine huenda vikakuumiza.

Mwigulu Nchemba Akizungumza:



Pia Waziri Mwigulu aliwataka Jeshi la Polisi kuhakikisha wanaanza kuwakamata wote wanaoagiza kufanyika maandamano nchi nzima.

Waziri aliyasema maneno hayo akiwaasa viongozi wa CHADEMA kutupilia mbali mpango wa maandamano na mikutano ya siasa nchi nzima Septemba Mosi mwaka huu.

Kufuatia kauli hiyo ya Waziri Mwigulu Lameck Nchemba, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) amemjibu wakati akizungumza kwenye kikao cha ndani cha chama hicho.


Sikiliza alichokisema Lema hapa:




Credits: Global Publishers
ZeroDegree.
AUDIO: Majibu ya Lema kwa Waziri Mwigulu kuhusu maandamano ya Septemba 1. AUDIO: Majibu ya Lema kwa Waziri Mwigulu kuhusu maandamano ya Septemba 1. Reviewed by Zero Degree on 8/22/2016 08:00:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.