Loading...

Fursa zilizopo katika Lugha ya Kiswahili.

Jana Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, alifanya uzinduzi wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira, Tanzania (Uwaridi) lengo kuu likuwa ni kurudisha usomaji wa riwaya za Kiswahili nchini pamoja na kupigania na kutetea maslahi ya waandishi wa riwaya za Kiswahili ambao kwa miaka mingi kazi zao zimeshindwa kuwanufaisha.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.
Utandawazi umeiathiri lugha ya Kiswahili kwa kiasi fulani kwani kwa sasa imekuwa kawaida kuchanganya lugha wakati wa mazungumzo jambo linaloifanya lugha hiyo kuathirika na kushindwa kukua haraka.

Kiswahili kinatoa fursa nyingi kwa wanaoikizungumza, ikiwemo kuutangaza utamaduni wa nchi. Mkurugezi Msaidizi Lugha Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo anasema kutumia Lugha ya Kiswahili kutasaidia kuendeleza na kuenzi juhudi za watetezi wa masuala ya lugha na utamaduni wa mtanzania.

Mbali na hilo pia Lugha ya Kiswahili inatoa fursa za ajira kupitia ukalimani na hata uandishi wa vitabu. Pia kwa wanaokifahamu vizuri Kiswahili na kuizungumza hurahisisha mawasiliano na shughuli za kibiashara kwani lugha ndio msingi wa mawasiliano baina ya mtu na mtu.

Credits: Mtembezi
ZeroDegree.
Fursa zilizopo katika Lugha ya Kiswahili. Fursa zilizopo katika Lugha ya Kiswahili. Reviewed by Zero Degree on 8/26/2016 11:39:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.