Loading...

Hatimaye Samatta aipeleka Genk hatua ya makundi Europa Ligi.

SAMATTA kaiongoza timu yake katika mchezo wa marudiano hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Europa Ligi dhidi ya Lokomotiva Zagreb ya Croatia. Mchezo umemalizika kwa Genk kutoka kifua mbele baada ya kuichakaza Lokomotiva zagreb goli mbili kwa sifuri.
Mchezo wa awali ulichezwa alihamis ya wiki iliyopita(Tar 18 mwezi huu) na matokeo yalikuwa ni sare ya 2-2, ambapo Samatta aliifungia timu yake(Genk) bao moja.

Samatta alikuwa wa kwanza kufumania nyavu leo katika mchezo wa marudiano uliomalizika hivi punde. Ilikua ni dakika ya pili tu ya mchezo ambapo Samatta alipachika bao hilo akipata assist kutoka kwa Bailey na kuipatia timu yake goli la kuongoza.

Goli la pili lilipatikana kipindi cha pili dakika ya 50 ya mchezo, mfungaji wa goli hilo akiwa ni Bailey ( aliyetoa assist ya goli la kwanza ) akipokea assist toka kwa Trossard.

Kwa matokeo hayo Genk inasonga mbele katika hatua ya makundi kwenye michoano hiyo ya EUROPA LIGI kwa jumla ya magoli manne ya michezo yote miwili nyumbani na ugenini huku wapinzani wao Lokomotima zagreb wakiambulia goli mbili za mchezo wa kwanza pekee ( Aggregate: KRC Genk 4 - Lok. Zagreb 2 ).
KRC Genk ya Samatta sasa inasubiri droo itakayochezeshwa August 26 Monaco nchini Ufaransa kusubiri itapangwa na vigogo gani kutoka ligi mbali mbali barani ulaya, miongoni mwa timu kubwa zitakazoshiriki katika hatua hiyo ya makundi Europa League ni pamoja na Man United ya Uingereza.

Matoke ya mechi nyingine(Zilizomalizika na zinazoendelea hadi hivi sasa):


ZeroDegree.
Hatimaye Samatta aipeleka Genk hatua ya makundi Europa Ligi. Hatimaye Samatta aipeleka Genk hatua ya makundi Europa Ligi. Reviewed by Zero Degree on 8/25/2016 11:19:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.