Loading...

Mzee Yusuf afichua mazito ya Jahazi.

ALIYEKUWA mfalme wa muziki wa taarabu nchini, Mzee Yusuf, amesema alijiondoa Ukurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarab miaka mitatu iliyopita ili kujiandalia mazingira rafiki ya kwenda kumwabudu kikamilifu mola wake.


Mzee Yusuf ambaye alikuwa mmiliki wa kundi hilo, aliwaambia wandishi wa habari kwamba, uamuzi wa kuachana na muziki alishauanika muda mrefu lakini watu wengi walikuwa hawaamini na kudhani alikuwa akitafuta kiki.

“Suala la kuacha muziki wa dunia nilikuwa nalo tangu mwaka 2013, mara kwa mara nilikuwa nikisema, lakini watu walijua natafuta umaarufu bila kujua namaanisha, ndio maana nilijivua ukurugenzi huku mimi na mke wangu Leyla tukiwa kama wafanyakazi wa kawaida,” alisema.

Alisema kwa sasa kundi hilo si mali yake na liko chini ya Rashidi Yusuf maarufu kama ‘Chiddy Boy’, Mohammed Mauji, maarufu ‘Gaza Mauji’ na Khadija Yusuf.

Aidha, Mzee Yusuf alisema alichelewa kujiondoa kundini kwa muda mrefu baada ya wasanii wa kundi hilo kumwomba awaelekeze baadhi ya vitu ili wapate pa kushika na muda ulipofika akafanya uamuzi huo mgumu.


Credits: Dimba
Zerodegree.
Mzee Yusuf afichua mazito ya Jahazi. Mzee Yusuf afichua mazito ya Jahazi. Reviewed by Zero Degree on 8/25/2016 09:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.