Loading...

Ibrahim Ajibu azidi kutupia magoli Simba SC.

MSHINDI wa tuzo ya bao bora la msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ibrahim Ajibu, ameendelea kudhihirisha kwamba yeye ndiye mfalme mpya wa mabao wa klabu hiyo.


Ajibu ambaye mashabiki wake wanamuita ‘Kadabra’ alidhihirisha hayo juzi jioni wakati Simba ikiendeleza wimbi la ushindi katika mechi za kujipima nguvu baada ya jana kuifunga Moro Kids mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Highlands, Bigwa mkoani Morogoro.

Huo unakuwa ushindi wa pili kwa Simba iliyoweka kambi katika Chuo cha Biblia mjini hapa kujiandaa na msimu mpya, baada ya Jumanne kuifunga mabao 6-0 Polisi Morogoro kwenye uwanja huo.

Mabao ya Simba iliyo chini ya kocha mpya, Mcameroon Joseph Marius Omog katika mchezo wa dhidi ya Moro Kids yalifungwa na Ajibu na Danny Lyanga.
Kwa Ajibu, alirudia kufunga baada ya Jumanne pia kufunga mara mbili katika ushindi wa 6-0, mabao mengine yakifungwa na mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Frederick Blagnon (mawili), Abdi Banda (moja) sawa na Mohammed Mussa.

ZeroDegree.
Ibrahim Ajibu azidi kutupia magoli Simba SC. Ibrahim Ajibu azidi kutupia magoli Simba SC. Reviewed by Zero Degree on 8/01/2016 10:31:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.