Loading...

Waamuzi FIFA wazuiwa hotelini.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas.

VIFAA vya waamuzi 30 wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) wanaoendelea na mafunzo yao Dar es Salaam vimezuiwa hotelini baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kudaiwa kiasi cha Sh milioni 9.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya waamuzi hao walisema kuwa awali wenyewe ndio walizuiwa kutoka katika hoteli hiyo (jina tunalo) baada ya deni hilo la TFF.

Mwamuzi mmoja (ambaye hakutaka jina lake litajwe) alisema kuwa baada ya TFF kulipa Sh milioni 2, uongozi wa hoteli hiyo iliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam ulikubali kuwaachia, lakini umebaki na mizigo yao yakiwemo masanduku na vifaa vya kujifunzia.

Alisema kuwa baada ya vifaa vyao kuzuiwa hawajui watatumia nini katika masomo yao, ambapo leo wataanza mitihani ya vitendo.

Taarifa kutoka TFF zinasema kuwa mmoja wa viongozi wa shirikisho hilo (jina tunalo) alipewa fedha hizo, lakini alichelewesha kuzifikisha hotelini hapo lakini baada ya kuzifikisha kila kitu kimeenda vizuri.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas alipoulizwa jana kuhusu suala hilo alisema anachojua yeye kuwa fedha zote zimelipwa katika hoteli hiyo na waamuzi hao walishaondoka.

Aliomba kupatiwa muda zaidi wa kulifanyia kazi suala hilo ili kutoa jibu la uhakika kwa vyombo vya habari.

Credits: Habari Leo
ZeroDegree.
Waamuzi FIFA wazuiwa hotelini. Waamuzi FIFA wazuiwa hotelini. Reviewed by Zero Degree on 8/01/2016 10:58:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.