Loading...

Lowassa aibukia Nanenane Moro

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa. 

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye chama chake cha Chadema kipo kwenye mgogoro na Serikali kuhusu kuzuiwa kwa mikutano ya hadhara juzi aliweka siasa kando wakati alipofanya ziara kwenye viwanja vya Nanenane mjini hapa na kutoa ushauri kuhusu kilimo.

Lowassa ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, ambayo hivi karibuni iliazimia kufanya mikutano ya hadhara na maandamano nchi nzima kupinga kile inachokiita ukandamizwaji wa demokrasia na udikteta, lakini hakutaka kuingiza siasa katika ziara yake kwenye mabanda yaliyoshiriki Maonyesha ya Nanenane Kanda ya Mashariki yaliyomalizika jana.

Akizungumza kwenye Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere mjini Morogoro mwishoni mwa ziara hiyo, Lowassa alishauri wananchi kutumia utafiti kuboresha kilimo ili kuwaletea manufaa.

Lowassa alieleza kuvutiwa na mafanikio na ubunifu kwenye sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi, akisema vijana wana nafasi kubwa kuwasilisha utafiti mbalimbali waliofanya katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi, ili wananchi wautumie kubadilisha kilimo cha mazoea na kuwa cha kisasa.


Credits: Mwananchi
ZeroDegree.
Lowassa aibukia Nanenane Moro Lowassa aibukia Nanenane Moro Reviewed by Zero Degree on 8/09/2016 07:58:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.