Viongozi Chadema wasota rumande saa 72
Viongozi wa Chadema Kanda ya Ziwa waliokamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za uchochezi wa kutumia mitandao ya kijamii wamesota rumande zaidi ya masaa 72 baada ya kunyimwa dhamana na kushindwa kufikishwa mahakamani.
Viongozi hao ambao ni Katibu wa Chadema kanda hiyo, Meshack Mecus na mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Geita, Neema Chozaile walikamatwa na jeshi la polisi Agosti 6 mwaka huu saa mbili asubuhi ambapo wamekaa rumande hadi leo saa tisa alasiri.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Mponjoli Mwabulambo alikiri viongozi hao kukaa rumande kwa siku tatu mfululizo na kusema walinyimwa dhamana kutokana na sababu za kiupelelezi.
“Ni kweli tuliwanyima dhamana kwa sababu za kiuchunguzi kwa kuwa tungewaachia wangeweza kuharibu uchunguzi na sasa tumewapa dhamana kwakua tayari upelelezi wetu umefika sehemu nzuri na tutawapandisha mahakamani wakati wowote tutakapokamilisha,” alisema.

Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Viongozi Chadema wasota rumande saa 72
Reviewed by Zero Degree
on
8/09/2016 07:59:00 AM
Rating: