Loading...

Matokeo ya Ligi Kuu ya Vodacom leo Tar 28 Agosti yako hapa, Yanga waanza vyema kutetea Ubingwa wao.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom 2015/2016, Yanga wametoka kifua mbele katika mchezo wao wa kwanza kwenye ligi kuu ya Vodacom leo Jumapili ya tar 28 Agosti dhidi ya African Lyon katika uwanja wa taifa.

Mchezo huo umemalizika kwa Yanga kujinyakulia pointi 3 muhimu baada ya kuifunga African Lyon goli 3-0, magoli ya Yanga yamefungwa na Deus Kaseke (dakika ya 18), wakati goli la pili likifungwa na Simon Msuva (dakika ya 59) na goli la tatu likifungwa na Juma Mahadhi katika dakika za nyongeza (dakika ya 90+2).

Baada ya mchezo huu wa leo ambao Yanga wamefanikiwa kuondoka na pointi zote tatu, mechi inaofuatia kwa Yanga itakukuwa dhidi ya JKT Ruvu inayotarajia kuchezwa Jumatano katika uwanja wa Taifa.

Mechi nyingine iliyochezwa leo Tar 28, Agosti ni ya Mbeya City dhidi ya Toto Africans ambapo 
Mbeya City imeibuka kidedea kwa ushindi wa goli 1 - 0, goli la Mbeya City limefungwa na Haruna Shamte katika dakika ya 6 ya mchezo.

ZeroDegree.

Matokeo ya Ligi Kuu ya Vodacom leo Tar 28 Agosti yako hapa, Yanga waanza vyema kutetea Ubingwa wao. Matokeo ya Ligi Kuu ya Vodacom leo Tar 28 Agosti yako hapa, Yanga waanza vyema kutetea Ubingwa wao. Reviewed by Zero Degree on 8/28/2016 07:28:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.