Loading...

Messi aondolewa katika TOP 3 ya wachezaji watakaowania tuzo ya mchezaji bora Ulaya.

Shirikisho la Soka Barani Ulaya, UEFA licha ya kuchezesha droo ya mechi za play offs za Ligi ya Mabingwa Ulaya, walitangaza majina matatu ya wachezaji wa waliofanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora barani Ulaya 2015/2016.


UEFA wamewatangaza wachezaji watatu wamliofanikiwa kuingia TOP 3, kati ya wachezaji 10 waliokuwa wamechaguliwa mwanzoni, Cristiano Ronaldo, Gareth Bale wote wa Real Madridna Mfaransa Antoinne Griezman wa Atletico Madrid ndio wamefanikiwa kuingia TOP 3.

Washiriki wengine 7 na point zao walioshindwa kuingia TOP 3.

Waandishi wa habari kutoka nchi 55 wanachama wa UEFA wanatarajiwa kupiga kura August 25 2016 kumchagua mchezaji bora wa UEFA kwa msimu wa 2015/2016.

ZeroDegree.
Messi aondolewa katika TOP 3 ya wachezaji watakaowania tuzo ya mchezaji bora Ulaya. Messi aondolewa katika TOP 3 ya wachezaji watakaowania tuzo ya mchezaji bora Ulaya. Reviewed by Zero Degree on 8/05/2016 10:21:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.