Loading...

Mfanyabiashara Mkoani Morogoro atiwa mbaroni baada ya kukutwa na fulana za Ukuta.

POLISI mkoani Morogoro linamshikilia mfanyabiashara wa nguo, Elils Samwel, maarufu kama Lema (40), mkazi wa Kihonda,Manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za kupatikana na fulana seti tisa zenye maandishi yanayosomeka ‘Ukuta Septemba mosi’.
Akizungumzia tukio hilo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, alisema mfanyabiashara huyo alikamatwa Agosti 19, mwaka huu, wakati polisi walipokuwa doria katika eneo hilo.

Alisema mfanyabiashara huyo alikutwa akiwa na fulana hizo zenye rangi nyekundu na nyeusi zikiwa na maandishi hayo yanayoaminika na kuashiria kuwa ni uchochezi dhidi ya serikali.

Mtuhumiwa huyo anaendelea kuhojiwa na polisi na atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika kwa kosa la kujihusisha na uchochezi dhidi ya serikali.

Katika hatua nyingine, polisi imekamata bunduki aina ya gobole Agosti 21, eneo la Mtawala, Manispaa ya Morogoro na mitambo ya kutengeneza bunduki kienyeji.

Aidha,Kamanda Matei, alisema polisi wamemkamata Mashaka Ramadhani, maarufu kama Mavumila, mkazi wa Chamwino kwa tuhuma za kuhusika na utengenezaji wa bunduki aina ya gobole na vifaa vya kutengeneza silaha hizo.

Kamanda Matei alisema, vifaa alivyokutwa navyo mtuhumiwa ni mabomba10, mtambo wa kuchochea moto, nati, vyuma, tupa, ubao, kitako cha bunduki, mfuniko wa bunduki, bunduki aina ya gobole na risasi tisa. Alisema, mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Credits: Nipashe
ZeroDegree.
Mfanyabiashara Mkoani Morogoro atiwa mbaroni baada ya kukutwa na fulana za Ukuta. Mfanyabiashara Mkoani Morogoro atiwa mbaroni baada ya kukutwa na fulana za Ukuta. Reviewed by Zero Degree on 8/24/2016 09:58:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.