Mjue Mtanzania aliyeweka historia katika michezo ya Olimpiki Nchini Brazili
Kwa mara ya kwanza katika historia ya michezo ya Olimpiki tangu mwaka 1980 baada ya Suleiman Nyambui na Filbert Bayi kufanya vizuri Moscow, Mtanzania Alphonce Simbu jana aliweka historia baada ya kushika nafasi ya tano katika mbio za marathon za kilometa 42.
Michezo hiyo iliyohitimishwa jana, ilikuwa ikifanyika kwenye Mji wa Rio de Janeiro, Brazil.
Katika mbio hizo zilizoanza mchana, Simbu angalau alionyesha tumaini jipya katika michezo ya Tanzania licha ya kukosa medali kwa kuonyesha bidii tangu mwanzo huku akiwaacha wanariadha zaidi ya 155 walioshiriki mbio hizo.
Simbu na wanariadha wengine wa Tanzania, Said Makula na Fabian Joseph ndio waliokuwa tegemeo la mwisho katika michezo hiyo baada ya wanamichezo wengine kutolewa hatua za awali. Makula alishika nafasi ya 43 wakati Fabian nafasi ya 112.

ZeroDegree.
Mjue Mtanzania aliyeweka historia katika michezo ya Olimpiki Nchini Brazili
Reviewed by Zero Degree
on
8/22/2016 11:30:00 AM
Rating: