Loading...

Bosi Usalama wa Taifa astaafu.

Rashid Othman
MKURUGENZI Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), Rashid Othman amestaafu rasmi wadhifa huo, huku akitajwa kuwa miongoni mwa viongozi waliofanya kazi nzuri wakiongoza taasisi hiyo nyeti.

Habari za uhakika kutoka ndani ya serikali, zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana, zilisema kuwa Othman alistaafu rasmi wadhifa huo Agosti 19, mwaka huu akiwa ameiongoza taasisi hiyo tangu Agosti 20, 2006 ikiwa ni takribani miaka 10.

Kiongozi huyo aliteuliwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kuwa Mkurugenzi Mkuu ili kuziba nafasi iliyoachwa na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa wakati huo, Cornel Apson Mwang’onda.

Aliapishwa Ikulu Dar es Salaam Agosti 21, 2006. Kabla ya uteuzi wake, Othman alikuwa Mkuu wa Utawala na Utumishi wa Idara hiyo ya Usalama wa Taifa na kufanya kazi nzuri, iliyochangia kumwezesha kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu.

Awali, Othman alitakiwa kustaafu mwaka 2013 kwa mujibu wa sheria, lakini aliendelea kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja mmoja hadi alipokubaliwa kustaafu rasmi Ijumaa iliyopita. Othman atakumbukwa kwa kazi nzuri, aliyoifanya kwa Taifa tangu alipoingia katika utumishi wa umma.

Wadau mbalimbali waliozungumza na gazeti hili jana, wamemtakia maisha mema na kila la kheri awapo mapumzikoni, huku wakisifu jitihada zake za kuifanya nchi kuendelea kuwa yenye amani na utulivu.


Source: Habari Leo
ZeroDegree.
Bosi Usalama wa Taifa astaafu. Bosi Usalama wa Taifa astaafu. Reviewed by Zero Degree on 8/22/2016 11:38:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.