Loading...

Mwanamke ajinyonga akiwa mahabusu.

Mahabusu Victoria Edward (51), mkazi wa Lemara mkoani hapa, aliyekuwa anatuhumiwa kuchoma moto nyumba ya familia yao, amejinyonga hadi kufa ndani ya chumba cha mahabusu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea katika Kituo cha Polisi cha Kati usiku wakati wenzake wakiwa wamelala.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo.
“Polisi wa zamu alisikia kelele kutoka kwenye chumba cha mahabusu wa kike, walijitahidi kuokoa maisha ya mahabusu, lakini ilishindikana,” alisema.

Mkumbo alisema mahabusu huyo alijinyonga kwa kutumia shuka alilokuwa anatumia kujifunika.

Alisema mtuhumiwa huyo alitarajiwa kupandishwa kizimbani kusomewa mashtaka yaliyokuwa yanamkabili jana.

Credits: Mwananchi
ZeroDegree.
Mwanamke ajinyonga akiwa mahabusu. Mwanamke ajinyonga akiwa mahabusu. Reviewed by Zero Degree on 8/25/2016 10:09:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.