Loading...

Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' awatoa hofu mashabiki wa hiyo.

'Cannavaro', amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo na kuwaahidi kuendeleza ubabe kwenye ligi kuu.

Akizungumza baada ya mazoezi ya jana,Cannavaro, alisema kutolewa kwao kwenye mashindano ya kimataifa sio kielelezo cha kuidharau timu hiyo. 

Alisema kuwa wanarejea kwenye ligi na hasira zao za kutolewa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika wataanza kuzishusha leo kwenye mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya African Lyon.

"Mashabiki wasiwe na hofu na timu yao...,tumetoka kwenye mashindano makubwana sasa tunarejea kwenye ligi kwa nguvu zote,"alisema Cannavaro.

Aidha, alisema kuwa mchezo wa leo kwao ni sehemu ya kuondoa machungu yao ya kushindwa kufuzu kwa hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

"Kuondolewa kimataifa aina maana kuwa tuna timu mbaya au wachezaji wamechoka.., mashabiki na wanachama watulie waje uwanjani kesho na tunawaaihidi furaha,"aliongezeaa kusema Cannavaro.

Cannavaro alikosa michezo miwili ya mwisho ya michuano hiyo ya Afrika kutokana na kuwa majeruhi.

ZeroDegree.
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' awatoa hofu mashabiki wa hiyo. Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' awatoa hofu mashabiki wa hiyo. Reviewed by Zero Degree on 8/28/2016 10:28:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.