Nay wa Mitego kuachia video ya wimbo wake wa ‘Pale Kati’ wiki hii.
Rapper Nay wa Mitego amedai ametimiza matakwa aliyopewa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) baada ya kufungiwa kwa wimbo wake wa ‘Pale Kati’, ambapo Jumatano hii taachia version ya kwanza ya video ya wimbo huo.
Nay amewataka mashabiki wake wa muziki wa kimataifa kukaa mkao wa kula.
“Mimi na BASATA tulishamalizana, wao walinipa maazimio na mimi nimeshayatekeleza, kwa hiyo na mimi naendelea na issue zingine,”alisema Nay.
“Jumatano hii mashabiki wangu Wakimataifa pamoja na wa kwenye mitandao ya kijamii wakae mkao wa kula, naachia video,”
Rapper huyo alisema wimbo wa ‘Pale Kati’ una nguvu kubwa sana na unafanya vizuri katika baadhi ya nchi kama Kenya, Uganda pamoja na Ghana, na ndio maana ameamua kuanza kutoa video kwa ajili ya kimataifa kwanza.
Pia amewataka mashabiki wa muziki wake kuendelea kusubiria mambo mazuri kwani wimbo huo una video nne.
- Baraza la Sanaa la Taifa [ BASATA ] limemfungia Nay wa Mitego kwa muda usiojulikana.
- BASATA yafungia nyimbo mpya ya NAY WA MITEGO, "Pale Kati".
“Mimi na BASATA tulishamalizana, wao walinipa maazimio na mimi nimeshayatekeleza, kwa hiyo na mimi naendelea na issue zingine,”alisema Nay.
“Jumatano hii mashabiki wangu Wakimataifa pamoja na wa kwenye mitandao ya kijamii wakae mkao wa kula, naachia video,”
Rapper huyo alisema wimbo wa ‘Pale Kati’ una nguvu kubwa sana na unafanya vizuri katika baadhi ya nchi kama Kenya, Uganda pamoja na Ghana, na ndio maana ameamua kuanza kutoa video kwa ajili ya kimataifa kwanza.
Pia amewataka mashabiki wa muziki wake kuendelea kusubiria mambo mazuri kwani wimbo huo una video nne.
ZeroDegree.
Nay wa Mitego kuachia video ya wimbo wake wa ‘Pale Kati’ wiki hii.
Reviewed by Zero Degree
on
8/09/2016 11:49:00 AM
Rating: